Hud 11:84
هودوَإِلَىٰ مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْبًا ۚ قَالَ يَـٰقَوْمِ ٱعْبُدُوا۟ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُۥ ۖ وَلَا تَنقُصُوا۟ ٱلْمِكْيَالَ وَٱلْمِيزَانَ ۚ إِنِّىٓ أَرَىٰكُم بِخَيْرٍ وَإِنِّىٓ أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ مُّحِيطٍ
Na kwa watu wa Madyana tuliwatumia ndugu yao Shu'aib. Akasema: Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna mungu yoyote isipokuwa Yeye, wala msipunguze vipimo na mizani. Mimi ninawaona mko katika hali njema, nami ninawahofia adhabu ya siku kubwa hiyo itakayowazingira.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kwa watu wa Madyana tuliwatumia ndugu yao Shua'ib. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye, wala msipunguze vipimo na mizani. Mimi nakuoneni mmo katika hali njema, nami nakukhofieni adhabu ya Siku kubwa hiyo itakayo kuzungukeni. [84]
[84] Na kwa watu wa Madyana tulimtuma ndugu yao kwa nasaba na mapenzi na kuoneana huruma, Shua'ib. Aliwaambia: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu Mmoja peke yake. Nyinyi hamna anaye stahiki kuabudiwa isipo kuwa Yeye. Wala msipunguze vipimo na mizani mnapo wauzia watu vitu vya kupimwa kwa pishi au kwa mizani. Hakika mimi nakuoneni ni watu wa kutarajiwa kheri kwa kumshukuru na kumt'ii Mwenyezi Mungu, na kuwapa watu haki zao kaamili. Na mimi nakukhofieni ikiwa hamtaishukuru kheri ya Mwenyezi Mungu na hamuitikii amri yake, isije ikakuteremkieni adhabu ya siku msio weza kuvikimbia vitisho vyake, kwa kuwa hivyo huwazinga wanao adhibiwa wasipate njia ya kusalimika. Hizi Aya mbili zinakataza kupunja kwa vipimo na mizani kwa kuwa ni ukhalifu unao stahiki kupewa adhabu na kuaziriwa. Makosa haya ya kupunja na udanganyifu pia yanahisabiwa ni ukhalifu hata katika kanuni za kutungwa za dikrii. Na katika Qur'ani tukufu ni moja katika njia ya kulinda mali. Nchi ya Madyana ipo baina ya kaskazi ya Hijazi na kusini ya Sham. Na hii ilikuwa imejaa miti. Ikiitwa Al-aykah,(yaani Machakani). Na Mwenyezi Mungu aliwapelekea adhabu kwa sababu ya uasi wao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tulimtuma kwenda kwa watu wa Madyan ndugu yao Shu‛ayb, akasema, «Enyi watu wangu, muabuduni Allah Mtukufu, Peke Yake. Nyinyi hamna mungu yoyote anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu, basi mtakasieni ibada. Wala msiwapunguzie watu haki zao katika vipimo vyao na mizani zao. Mimi nawaona nyinyi mko kwenye ukunjufu wa maisha, na mimi nawachelea, kwa sababu ya kupunguza vipimo na mizani, adhabu ya siku itakayowazunguka».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net