Hud 11:83
هودمُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَ ۖ وَمَا هِىَ مِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ بِبَعِيدٍ
Zilizotiwa alama kwa Mola wako Mlezi. Na haya hayako mbali na madhalimu wengineo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Zilizo tiwa alama kwa Mola wako Mlezi. Na haya hayako mbali na wenye kudhulumu wengineo. [83]
[83] Wakawa wanaangukiwa na hayo mawe mfululizo kuwa ni adhabu inayo toka kwa Mola wako Mlezi, ewe Nabii! Na hayo si mbali kumfikilia kila mwenye kudhulumu katika kaumu yako.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
yamewekwa alama huko kwa Allah Mtukufu kwa alama inayojulikana, hayafanani na majiwe yaliyo ardhini. Na hayakuwa majiwe haya ambayo Allah Mtukufu aliwateremshia watu wa Lût, yako mbali na makafiri wa kikureshi kuwa watateremshiwa mfano wake. Katika haya kuna onyo kwa kila aliyeasi aliyeshindana na Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net