Hud 11:82
هودفَلَمَّا جَآءَ أَمْرُنَا جَعَلْنَا عَـٰلِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهَا حِجَارَةً مِّن سِجِّيلٍ مَّنضُودٍ
Basi ilipokuja amri yetu, tuliigeuza nchi juu chini, na tukaiteremshia mvua ya changarawe za udongo mgumu uliokamatana wa Motoni.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi ilipo fika amri yetu tuliigeuza nchi juu chini, na tukawateremshia mvua ya changarawe za udongo mgumu ulio kamatana wa Motoni, [82]
[82] Ulipo fika wakati wa adhabu tuliyo ikadiria na tukaitolea hukumu, tuliupindua mji ule walio kuwa wakiishi ndani kaumu Lut' juu chini. Na tukawanyeshea mvua ya mawe ya udongo ulio okwa Motoni hata ukawa changarawe!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi amri yetu ilipokuja, ya adhabu kuwashukia, tuliifanya sehamu ya juu ya kijiji chao ambayo walikuwa wakiishi juu yake kuwa chini kwa kukigeuza. Na tuliwateremshia majiwe ya udongo ulio mgumu wenye nguvu, yamepangwa baadhi yake juu ya mengine na yamefuatana,
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net