Hud 11:81
هودقَالُوا۟ يَـٰلُوطُ إِنَّا رُسُلُ رَبِّكَ لَن يَصِلُوٓا۟ إِلَيْكَ ۖ فَأَسْرِ بِأَهْلِكَ بِقِطْعٍ مِّنَ ٱلَّيْلِ وَلَا يَلْتَفِتْ مِنكُمْ أَحَدٌ إِلَّا ٱمْرَأَتَكَ ۖ إِنَّهُۥ مُصِيبُهَا مَآ أَصَابَهُمْ ۚ إِنَّ مَوْعِدَهُمُ ٱلصُّبْحُ ۚ أَلَيْسَ ٱلصُّبْحُ بِقَرِيبٍ
(Wajumbe) wakasema: Ewe Lut! Sisi ni wajumbe wa Mola wako Mlezi. Hawa hawatakufikia. Basi wewe ondoka pamoja na ahali zako usiku ungalipo. Wala yeyote miongoni mwenu asitazame nyuma, isipokuwa mkeo, kwani yeye utamfika msiba utakaowafika hao. Hakika miadi yao ni asubuhi. Je, kwani asubuhi haiko karibu sana?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
(Wajumbe) wakasema: Ewe Lut'! Sisi ni wajumbe wa Mola wako Mlezi. Hawa hawatakufikia. Na wewe ondoka pamoja na ahali zako usiku ungalipo. Wala yeyote miongoni mwenu asitazame nyuma, isipo kuwa mkeo, kwani yeye utamfika msiba utakao wafika hao. Hakika miadi yao ni asubuhi. Je, asubuhi si karibu? [81]
[81] Malaika wale wakamwambia, na wao ukweli wao ulikwisha dhihiri: Ewe Lut'! Usikhofu wala usihuzunike! Sisi ni wajumbe wa Mola wako Mlezi, wala si binaadamu kama tuonekanavyo kwako na kwa hawa kaumu yako. Wala wao hawa hawatakufikishia shari yoyote ya kukuudhi au kukudhuru. Basi toka wewe na ahali zako usiku ukisha zagaa. Mtoke mji huu, wala yeyote katika nyinyi asigeuke kutazama nyuma, asije akaona vitisho vya adhabu naye akasibiwa na shari yake! Lakini mkeo ambaye amekukhuni, yeye hatokuwa pamoja na watao toka nawe. Yeye lazima yampate yatao wapata hawa watu. Na miadi ya kuangamia kwao ni asubuhi, na miadi hiyo ni karibu. Basi usitie khofu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Malaika wakasema, Ewe Lûṭ, sisi ni wajumbe wa Mola wako, Ametutuma kuwaangamiza watu wako, na wao hawatakufikia. Basi toka kwenye kijiji hiki, wewe na watu wako (waliokuamini), katika kipindi kilichosalia cha usiku, na asigeuke nyuma yoyote katika nyinyi, ili asiione adhabu ikampata. Lakini mke wako aliyeenda kinyume chako kwa kukanusha na kufanya unafiki, kitampata yeye kile kitakachowapata watu wako cha maangamivu. Hakika maagano ya kuangamia kwao ni wakati wa asubuhi, nao ni wakati ambao ni karibu kufika.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net