Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 80

Hud 11:80

هود

قَالَ لَوْ أَنَّ لِى بِكُمْ قُوَّةً أَوْ ءَاوِىٓ إِلَىٰ رُكْنٍ شَدِيدٍ

Maana

Akasema: Laiti ningelikuwa na nguvu dhidi yenu, au nijilinde kwenye nguzo yenye nguvu!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Akasema: Laiti ningeli kuwa na nguvu kwenu, au nategemea kwenye nguzo yenye nguvu! [80]

[80] Lut' akasema: Laiti ningeli kuwa nina nguvu au nina nguzo yenye nguvu ya kutegemea, msimamo wangu juu yenu ungeli kuwa mwengine, na ningeli weza kuwalinda wageni wangu nikakuzueni msiwafanye mambo mabaya.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Walipokataa isipokuwa kufanya machafu, aliwaambia, «Lau ningekua na nguvu kwenu na nina wasaidizi pamoja na mimi, au ningetegemea ukoo utakaonihami na nyinyi, ningaliwazuia nyinyi na hayo mnayoyataka».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net