Hud 11:79
هودقَالُوا۟ لَقَدْ عَلِمْتَ مَا لَنَا فِى بَنَاتِكَ مِنْ حَقٍّ وَإِنَّكَ لَتَعْلَمُ مَا نُرِيدُ
Wakasema: Bila shaka umekwishajua hatuna haki yoyote juu ya binti zako, na hakika wewe unayajua yale tunayoyataka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wakasema: Bila shaka umekwisha jua hatuna haki juu ya binti zako, na unayajua tunayo yataka. [79]
[79] Wakasema: Wajua vyema ewe Lut', kuwa sisi hatuna haki ya kuwaoa binti zako, wala hatuwataki. Na wewe hapana shaka unajua tukitakacho tulipo kujia kwa haraka.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wakasema watu wa Lût kumwambia yeye, «Umeshajua tangu mbeleni kwamba sisi hatuna haja ya wanawake wala matamanio. Na wewe unajua tulitakalo. Yaani, sisi hatutaki isipokuwa wanaume na hatuna hamu ya kuoa wanawake».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net