Hud 11:78
هودوَجَآءَهُۥ قَوْمُهُۥ يُهْرَعُونَ إِلَيْهِ وَمِن قَبْلُ كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ ٱلسَّيِّـَٔاتِ ۚ قَالَ يَـٰقَوْمِ هَـٰٓؤُلَآءِ بَنَاتِى هُنَّ أَطْهَرُ لَكُمْ ۖ فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَلَا تُخْزُونِ فِى ضَيْفِىٓ ۖ أَلَيْسَ مِنكُمْ رَجُلٌ رَّشِيدٌ
Wakamjia kaumu yake mbio mbio. Na kabla ya haya walikuwa wakitenda mabaya. Yeye akasema: Enyi kaumu yangu! Hawa binti zangu, ndio wametakasika zaidi kwenu. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, wala msinihizi mbele ya wageni wangu. Hivyo je, hakuna hata mwanamume mmoja miongoni mwenu aliyeongoka?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wakamjia kaumu yake mbio mbio. Na kabla ya haya walikuwa wakitenda maovu. Yeye akasema: Enyi watu wangu! Hawa binti zangu, ndio wametakasika zaidi kwenu. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, wala msinihizi mbele ya wageni wangu. Hivyo, hamna hata mtu mmoja miongoni mwenu aliye ongoka? [78]
[78] Watu wake wakajua kuwa wamekuja wale wageni, wakamwendea mbio mbio. Na kabla ya hayo ilikuwa kazi yao kufanya huo uchafu wao na kutenda maovu! Lut' akawaambia: Enyi watu wangu! Hawa binti zangu, waoeni. Hao ni safi zaidi kwenu kuliko kwenda kufanya uchafu kwa wanaume! Mwogopeni Mwenyezi Mungu, na jilindeni nafsi zenu na adhabu yake; na msinifedhehi na mkanidharaulisha kwa kuwavamia wageni wangu! Basi hivyo hamna kati yenu hata mtu mmoja mwenye rai iliyo sawa, mwenye akili iliyo ongoka, akakuzuieni na maasi na akakukatazeni maovu?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Watu wa Lût wakamjia kwa haraka kutaka kufanya uchafu, na kabla ya kuja kwao walikuwa wanawaendea wanaume kwa njia ya matamanio badala ya wanawake. Lût akasema kuwaambia watu wake, «Hawa ni watoto wangu wa kike, waoeni. Wao ni wasafi zaidi kwenu kuliko hayo mnayoyataka.» Aliwaita kuwa ni watoto wake wa kike sababu Nabii wa ummah ana daraja ya baba kwao. «Basi muogopeni Allah Mtukufu na mjihadhari na mateso Yake, wala msinifedhehi kwa kuwakosea wageni wangu. Kwani hakuna mtu yoyote katika nyinyi aliye mzuri wa kupima mambo apate kuwakataza wanaotaka kufanya machafu akawzuia wao na hayo? Kumdhalilisha mgeni ni jambo la kutukanisha hakuna alifanyalo isipokuwa ni watu wa utwevu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net