Hud 11:77
هودوَلَمَّا جَآءَتْ رُسُلُنَا لُوطًا سِىٓءَ بِهِمْ وَضَاقَ بِهِمْ ذَرْعًا وَقَالَ هَـٰذَا يَوْمٌ عَصِيبٌ
Na wajumbe wetu walipomjia Lut, yakamuwia mabaya kwa sababu yao na akaona dhiki kubwa kwa sababu yao. Akasema: Hii ni siku ngumu sana!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wajumbe wetu walipo kuja kwa Lut' aliwahuzunukia na akawaonea dhiki. Akasema: Hii leo ni siku ngumu! [77]
[77] Walipo kuja wajumbe wetu, hao Malaika, kwa Lut' kwa sura ya vijana wazuri, Lut' aliungulika na akaudhika. Alihisi unyonge hana nguvu za kuwahami na hao watu wake, akawaonea dhiki kwa kuwaogopea ufisadi wa kaumu yake! Akasema: Hii leo ni siku ya karaha kubwa na machungu!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Malaika wetu walipomjia Lûṭ, aliudhika kwa kuja kwao na akaingiwa na hamu kwa hilo. Hivyo ni kwa kuwa yeye hakuwa anajua kwamba wao ni wajumbe wa Allah Mtukufu, akawachelea wasidhuriwe na watu wake na akasema, «Hii ni siku ya mtihani na shida».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net