Hud 11:76
هوديَـٰٓإِبْرَٰهِيمُ أَعْرِضْ عَنْ هَـٰذَآ ۖ إِنَّهُۥ قَدْ جَآءَ أَمْرُ رَبِّكَ ۖ وَإِنَّهُمْ ءَاتِيهِمْ عَذَابٌ غَيْرُ مَرْدُودٍ
(Akaambiwa): Ewe Ibrahim! Achilia mbali haya! Hakika amri ya Mola wako Mlezi imekwishakuja, na hakika hao itawafikia adhabu isiyorudishwa nyuma.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
(Akaambiwa): Ewe Ibrahim! Wachilia mbali haya! Kwa hakika amri ya Mola wako Mlezi imekwisha kuja, na hakika hao itawafikia adhabu isiyo rudi nyuma. [76]
[76] Malaika wakasema: Ewe Ibrahim! Wachilia mbali haya majadiliano, na kuwatakia rehema watu hawa. Kwani amri ya Mola wako Mlezi ya kuwaangamiza imekwisha kuja! Hapana budi kuwa adhabu itawashukia, na wala haitarudishwa kwa majadiliano au bila ya majadiliano.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wajumbe wa Allah Mtukufu wakasema, «Ewe Ibrãhîm, uache mjadala huu kuhusu mambo ya watu wa Lûṭ na kuwaombea huruma, kwani hakika ya mambo ni kwamba imethibiti juu yao adhabu na amri ya Mola wako aliyowapangia. Na wao, adhabu inayotoka kwa Allah Mtukufu ni yenye kuwashukia, si yenye kuepushwa na wao wala kuzuiliwa».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net