Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 75

Hud 11:75

هود

إِنَّ إِبْرَٰهِيمَ لَحَلِيمٌ أَوَّٰهٌ مُّنِيبٌ

Maana

Hakika Ibrahim alikuwa mvumilivu sana, mwenye huzuni kubwa, na mwepesi wa kurejea kwa Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika Ibrahim alikuwa mpole, ana huruma, na mwepesi wa kurejea kwa Mwenyezi Mungu. [75]

[75] Hakika Ibrahim ni mpole mno, hapendelei mapatilizo ya kwa haraka, mwingi wa kuungulika na kuona uchungu kwa shida zinao wapata watu, tena yeye ni mwenye kutubu na kurejea kwa Mwenyezi Mungu kwa yale ayapendayo na kuyaridhi. Basi ule upole wake, na rehema zake, na huruma zake ndizo zilizo mpelekea kubishana kule kwa kutaraji kuwa asaa Mwenyezi Mungu akawaondolea adhabu watu wa Lut', na wao wapate kutubu na kurejea kwake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika Ibrãhîm ni mwingi wa upole, hapendi uharakishaji wa adhabu, ni mwingi wa kunyenyekea kwa Allah Mtukufu na kumuomba, ni mwenye kutubia, anarejea kwa Allah Mtukufu katika mambo yake yote.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net