Hud 11:72
هودقَالَتْ يَـٰوَيْلَتَىٰٓ ءَأَلِدُ وَأَنَا۠ عَجُوزٌ وَهَـٰذَا بَعْلِى شَيْخًا ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَشَىْءٌ عَجِيبٌ
Akasema, "Ole wangu! Mimi nizae ilhali mimi ni ajuza? Na tena huyu mume wangu ni mzee? Hakika haya ni mambo ya ajabu!"
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akasema: Je, hivyo mimi nizae, na hali yangu ni kikongwe na huyu mume wangu ni kizee? Hakika haya ni mambo ya ajabu! [72]
[72] Mke wa Ibrahim alipiga ukelele kwa kustaajabu: Ajabu gani hii, jamani! Nizae mimi kikongwe, na huyu mume wangu mnamuona kesha kuwa kizee kabisa! Kama huyu hapati mwana tena. Hakika haya ninayo yasikia ni mambo ya ajabu. Vipi vikongwe viwili kama mimi na mume wangu wazae tena?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Alipopewa bishara ya Isḥãq, Sãrah alisema kwa kustaajabu, «Ee mimi ee! Vipi nitakuwa na mtoto na mimi ni mkongwe na huyu mume wangu yuko katika hali ya uzee na utu uzima? Kuzaa kwa mtu mfano wangu mimi na mfano wa mume wangu pamoja na ukuu wa miaka ni jambo la ajabu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net