Hud 11:73
هودقَالُوٓا۟ أَتَعْجَبِينَ مِنْ أَمْرِ ٱللَّهِ ۖ رَحْمَتُ ٱللَّهِ وَبَرَكَـٰتُهُۥ عَلَيْكُمْ أَهْلَ ٱلْبَيْتِ ۚ إِنَّهُۥ حَمِيدٌ مَّجِيدٌ
Wakasema: Je, unastaajabia amri ya Mwenyezi Mungu? Rehema ya Mwenyezi Mungu na baraka zake ziwe juu yenu, enyi watu wa nyumba hii! Hakika Yeye ndiye Msifiwa, Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wakasema: Je, unastaajabia amri ya Mwenyezi Mungu? Rehema ya Mwenyezi Mungu na baraka zake ziko juu yenu, enyi watu wa nyumba hii! Hakika Yeye ndiye Msifiwa wa kutukuzwa. [73]
[73] Malaika wakamwambia: Unastaajabu nyinyi wawili kupata mwana kwa ajili ya uzee wenu? Haya yanatokana na amri ya Mwenyezi Mungu asiye shindwa na chochote. Hiyo ndiyo rehema ya Mwenyezi Mungu. Na neema zake ni nyingi juu yenu wa ukoo wa Nabii. Basi hapana la ajabu nyinyi kupewa wasio pewa wenginewe. Mwenye kutenda hayo hakika anastahiki kuhimidiwa, ni mwingi wa hisani na ukarimu na upaji.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wajumbe walisema kumwambia, «Hivi wewe unaionea ajabu amri ya Allah Mtukufu na hukumu Yake? Rehema za Allah Mtukufu na baraka Zake ziwashukie nyinyi, enyi watu wa nyumba ya unabii. Hakika Yeye, kutakasika na kutukuka ni Kwake, ni mhimidiwa wa sifa na vitendo, ni Mwenye utukufu na ukubwa katika hizo».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net