Hud 11:71
هودوَٱمْرَأَتُهُۥ قَآئِمَةٌ فَضَحِكَتْ فَبَشَّرْنَـٰهَا بِإِسْحَـٰقَ وَمِن وَرَآءِ إِسْحَـٰقَ يَعْقُوبَ
Na mkewe alikuwa amesimama wima, akacheka. Basi tukambashiria kuhusu (kuzaliwa kwa) Is-haq, na baada ya Is-haq, Yaaqub.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na mkewe alikuwa kasimama wima, akacheka. Basi tukambashiria (kuzaliwa) Is-haq, na baada ya Is-haq Yaaqub. [71]
[71] Na mkewe alikuwa kasimama karibu akisikia maneno yao. Akacheka kwa furaha ya kuwa mwenyewe Lut', ambaye ni mtoto wa ndugu wa mumewe, atasalimika. Basi Sisi tulimbashiria kwa ndimi za wale Malaika kuwa atamzalia mumewe Ibrahimu mtoto mwanamume ataye itwa Is-haq, na huyo mtoto ataishi, na baadae Is-haq atampata Yaaqub.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Sãrah, mke wa Ibrãhîm, alikuwa amesimama nyuma ya pazia yuwasikia hayo maneno. Alicheka kwa kuyaonea ajabu aliyoyasikia. Hapo tukampa habari njema, kupitia kwa ndimi za Malaika, kwamba atazaa, kwa mume wake Ibrãhîm, mtoto atakayeitwa Isḥãq; na mtoto wake ataishi, na baada ya Isḥāq atakuwa na mjukuu kutoka kwake, naye ni Ya‛qûb.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net