Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 70

Hud 11:70

هود

فَلَمَّا رَءَآ أَيْدِيَهُمْ لَا تَصِلُ إِلَيْهِ نَكِرَهُمْ وَأَوْجَسَ مِنْهُمْ خِيفَةً ۚ قَالُوا۟ لَا تَخَفْ إِنَّآ أُرْسِلْنَآ إِلَىٰ قَوْمِ لُوطٍ

Maana

Basi alipoiona mikono yao haimfikii, akawatilia shaka, na akawahofu. Wakasema, "Usihofu! Hakika sisi tumetumwa kwa kaumu ya Lut."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi alipoona mikono yao haimfikilii aliwatilia shaka, na akawaogopa. Wakasema: Usiogope! Hakika sisi tumetumwa kwa kaumu ya Lut'. [70]

[70] Alipoona kuwa hawanyooshi mikono yao kama ada ya wageni akawatilia shaka kuwa hawa si wageni wa kawaida, na akahisi kuwa hawa ni Malaika. Ikamjia khofu kuwa isije kuwa kuja kwao ni kwa jambo ambalo halikumpendeza Mwenyezi Mungu, au kuwaadhibu watu wake. Wakasema, nao walijua athari ya ile khofu katika nafsi yake: Usiogope! Hakika sisi tumetumwa kuwahiliki kaumu Lut'.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Alipoona Ibrãhîm kuwa mikono yao haifikishwi kwenye yule ndama aliyewaletea na kuwa wao hawamli, alikataa hilo kutoka kwao na akaingiwa na hisia ya uoga ndani ya moyo wake. Malaika wakasema, walipoona uoga uliomuingia Ibrãhîm, «Usiogope! Sisi ni Malaika wa Mola wako tumetumwa kwenda kwa watu wa Lûṭ kuwaangamiza».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net