Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 69

Hud 11:69

هود

وَلَقَدْ جَآءَتْ رُسُلُنَآ إِبْرَٰهِيمَ بِٱلْبُشْرَىٰ قَالُوا۟ سَلَـٰمًا ۖ قَالَ سَلَـٰمٌ ۖ فَمَا لَبِثَ أَن جَآءَ بِعِجْلٍ حَنِيذٍ

Maana

Na hakika wajumbe wetu walimjia Ibrahim kwa bishara njema, wakasema, "Salama!" Naye akasema, "Salama!" Kisha hakukaa isipokuwa mara hiyo akaja na ndama wa kuchoma.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wajumbe wetu walimjia Ibrahim kwa bishara njema, wakasema: Salama! Naye akasema: Salama! Hakukaa ila mara akaleta ndama wa kuchoma. [69]

[69] Na Sisi tuliwatuma Malaika kwa Ibrahim wampe bishara njema yeye na mkewe kuwa watapata mwana. Waliwasalimu kwa kauli ya: Salama! Naye akarejesha amkio lao kwa kusema: Salama! Upesi upesi akenda kuwatengezea ndama aliye nona wa kuchoma ili wale.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika Malaika walimjia Ibrãhîm, amani imshukie, wakimpa yeye na mke wake bishara ya Isḥḥḥãq na Ya‛qûb baada yake, wakasema, «Salãm (amani)» Akasema kuwarudishia maamkuzi yao, «Salãm (amani)» Hapo akaondoka haraka na akarudi na ndama wa kuchoma aliyenona ili wao wale.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net