Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 68

Hud 11:68

هود

كَأَن لَّمْ يَغْنَوْا۟ فِيهَآ ۗ أَلَآ إِنَّ ثَمُودَا۟ كَفَرُوا۟ رَبَّهُمْ ۗ أَلَا بُعْدًا لِّثَمُودَ

Maana

Kama kwamba hawakuishi huko kwa ustawi. Hebu zingatieni! Hakika kina Thamud walimkufuru Mola wao Mlezi. Hebu zingatieni! Thamud walipotelea mbali!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kama kwamba hawakuwako huko. Hebu zingatieni! Hakika kina Thamud walimkufuru Mola wao Mlezi. Hebu zingatieni! Thamud wamepotelea mbali! [68]

[68] Mambo yao yakawaishia, na alama zao zikaondoka katika majumba yao. Wakawa kama kwamba hawajapata kuwamo humo. Hali yao ni ya kumzindua kila mwenye akili azingatie, na ajue kuwa hao kaumu ya Thamud walizikanya Ishara za aliye waumba!! Na kwa sababu ya hayo ndio wakaangamizwa na wakatengwa mbali na rehema ya Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kana kwamba wao, kwa haraka ya kuondoka kwao na kutoeka kwao, hawakuishi humo. Jueni mtanabahi kwamba Thamûd walikanusha aya za Mola wao na hoja Zake. Jueni mtanabahi kwamba kuwa mbali na kufukuzwa kwenye rehema za Allah Mtukufu ni kwa hao Thamûd; ni upotevu ulioje na unyonge ulioje huo wao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net