Hud 11:67
هودوَأَخَذَ ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ ٱلصَّيْحَةُ فَأَصْبَحُوا۟ فِى دِيَـٰرِهِمْ جَـٰثِمِينَ
Na ukelele uliwaangamiza wale waliodhulumu, basi wakawa majumbani mwao wamekufa kifudifudi!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ukelele uliwaangamiza wale walio dhulumu, wakapambazukiwa nao ni maiti majumbani mwao. [67]
[67] Ukelele uliwatwaa kina Thamud kwa nguvu zake, na tetemeko lake, na ngurumo lake, kwa kuwa hao walijidhulumu wenyewe kwa ukafiri wao na uadui. Kulipo pambazuka wakawa katika majumba yao kimya, wamejinyoosha kifudifudi, maiti, hawatweti!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na ukelele wa nguvu uliwapata Thamûd walio madhalimu, hapohapo wakawa kwenye majumba yao ni wafu waliokauka na kuanguka kwa nyuso zao, hakuna anayetikisika.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net