Hud 11:66
هودفَلَمَّا جَآءَ أَمْرُنَا نَجَّيْنَا صَـٰلِحًا وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مَعَهُۥ بِرَحْمَةٍ مِّنَّا وَمِنْ خِزْىِ يَوْمِئِذٍ ۗ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ ٱلْقَوِىُّ ٱلْعَزِيزُ
Basi ilipokuja amri yetu, tulimwokoa sawasawa Saleh na wale walioamini pamoja naye kwa rehema yetu kutokana na hizaya ya siku ile. Hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu, Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi ilipo kuja amri yetu tulimwokoa Swaleh na wale walio amini pamoja naye kwa rehema yetu kutokana na hizaya ya siku ile. Hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kushinda. [66]
[66] Ilipo kuja adhabu yetu tulimwokoa Swaleh na wale walio amini pamoja naye kutokana na maangamizo kwa rehema iliyo toka kwetu khasa. Na tukawaokoa na hizaya na fedheha ya siku ya maangamizo ya Thamud. Hakika Mola wako Mlezi, ewe Nabii, ni Mwenye nguvu na Mwenye kushinda. Basi tuwa ukitegemea nguvu zake, na ushindi wake, na msaada wake, na nusra yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi amri yetu ilipokuja ya kuwaangamiza Thamûd, tulimuokoa Ṣãliḥ na walioamini pamoja na yeye na maangamivu kwa rehema kutoka kwetu. Na tuliwaokoa wao na unyonge wa Siku hiyo na udhalilifu wake. Hakika Mola wako, ewe Mtume, Ndiye Mwenye nguvu, Mwenye ushindi. Na miongoni mwa nguvu Zake na ushindi Wake ni kuwa Aliwaangamiza watu wenye kupita kiasi kwenye uasi na akawaokoa Mitume na wafuasi wao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net