Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 65

Hud 11:65

هود

فَعَقَرُوهَا فَقَالَ تَمَتَّعُوا۟ فِى دَارِكُمْ ثَلَـٰثَةَ أَيَّامٍ ۖ ذَٰلِكَ وَعْدٌ غَيْرُ مَكْذُوبٍ

Maana

Lakini wakamchinja. Basi (Saleh) akasema: Stareheni katika makazi yenu (muda wa) siku tatu. Hiyo ni ahadi isiyokuwa ya uongo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wakamchinja. Basi (Swaleh) akasema: Stareheni katika mji wenu muda wa siku tatu. Hiyo ni ahadi isiyo kuwa ya uwongo. [65]

[65] Na wao wasiisikie nasaha yake, wala wasimkubalie. Kiburi chao na dharau yao iliwapelekea kumuuwa yule ngamia. Basi yeye akawaambia: Stareheni na maisha yenu ya kilimwengu katika miji yenu muda wa siku tatu. Kisha baadae itakujieni adhabu ya Mwenyezi Mungu. Hiyo ni ahadi ya kweli wala haina kinyume, wala haina uwongo ndani yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wakamkanusha na wakamchinja ngamia, hapo Ṣãliḥ akawaambia, «Stareheni na maisha yenu katika mji wenu kwa muda wa siku tatu, kwani adhabu ni yenye kuwashukia baada yake, na hiyo ni ahadi kutoka kwa Allah Mtukufu isiyokanushika, haina budi kutokea».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net