Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 64

Hud 11:64

هود

وَيَـٰقَوْمِ هَـٰذِهِۦ نَاقَةُ ٱللَّهِ لَكُمْ ءَايَةً فَذَرُوهَا تَأْكُلْ فِىٓ أَرْضِ ٱللَّهِ وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوٓءٍ فَيَأْخُذَكُمْ عَذَابٌ قَرِيبٌ

Maana

Na enyi kaumu yangu! Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu awe Ishara kwenu. Basi mwacheni ale katika ardhi ya Mwenyezi Mungu, wala msimguse kwa ubaya, ikaja kuwaangamiza adhabu iliyo karibu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi watu wangu! Huyu ngamia wa Mwenyezi Mungu ni Ishara kwenu. Basi mwacheni ale katika ardhi ya Mwenyezi Mungu; wala ms!imguse kwa ubaya, isije ikakuangamizeni adhabu iliyo karibu. [64]

[64] Na enyi watu wangu! Huyu ngamia wa Mwenyezi Mungu; amemfanya awe ni alama kwenu ya kushuhudia ukweli wa haya ninayo kuleteeni. Kwani huyu ni namna mbali na hao mlio wazoea. Basi mwachieni ale katika ardhi ya Mwenyezi, kwani yeye ni ngamia wake, na ardhi ni yake. Wala msimfikishie uovu wowote wa kumdhuru. Kwani mkifanya hivyo Mwenyezi Mungu atakuangamizeni kwa adhabu iliyo karibu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na enyi watu wangu, huyu ni ngamia wa Allah Mtukufu, Amemjaalia ni hoja na alama ya kuonesha ukweli wangu katika yale ninayowaitia. Basi muacheni ale katika ardhi ya Mawenyezi Mungu, kwani chakula chake hakiko juu yenu. Na wala msimguse kumchinja, kwani nyinyi mkifanya hivyo itawapata adhabu kutoka Kwake kwa muda mfupi baada kumchinja.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net