Hud 11:63
هودقَالَ يَـٰقَوْمِ أَرَءَيْتُمْ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّى وَءَاتَىٰنِى مِنْهُ رَحْمَةً فَمَن يَنصُرُنِى مِنَ ٱللَّهِ إِنْ عَصَيْتُهُۥ ۖ فَمَا تَزِيدُونَنِى غَيْرَ تَخْسِيرٍ
Akasema: Enyi kaumu yangu! Mnaonaje ikiwa ninao ushahidi ulio wazi kutoka kwa Mola wangu Mlezi, naye akawa amenipa rehema kutoka kwake, je, ni nani atakayeninusuru kutokana na Mwenyezi Mungu nikimuasi? Basi nyinyi hamnizidishii isipokuwa kuhasirika tu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akasema: Enyi watu wangu! Mwaonaje ikiwa ninazo dalili zilizo wazi kutokana na Mola wangu Mlezi, naye akawa kanipa rehema kutoka kwake - je, ni nani atakaye ninusuru kwa Mwenyezi Mungu nikimuasi? Basi nyinyi hamtanizidishia ila khasara tu. [63]
[63] Akasema: Enyi watu wangu! Hebu nambieni: ikiwa mimi kwa haya ninayo kukuitieni kwayo nina ujuzi nayo vilivyo, na nina hoja za kunitia nguvu kutoka kwa Mola wangu Mlezi, na ikawa Mola wangu Mlezi kanipa mimi na nyinyi rehema itokayo kwake, nayo ni Unabii na Utume, vipi basi nende kinyume na amri yake, na nimuasi kwa kutofikisha ujumbe wake kwa sababu ya kukusikilizeni nyinyi? Na nani wa kuninusuru na kunisaidia kuikinga adhabu yake nikimuasi Yeye? Nyinyi hamwezi kuninusuru na kunikinga na adhabu yake. Basi hamtonizidishia ila kupotea na kuingia khasarani ni kikut'iini nyinyi, na nikamuasi Mola wangu na Mola wenu Mlezi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ṣãliḥ akasema kuwaambia watu wake, «Enyi watu wangu, iwapo niko kwenye hoja ya Allah Mtukufu na ukanijia mimi utume na hekima kutoka Kwake, niambieni mimi: ni nani atakayeniondolea adhabu ya Allah Mtukufu nikimuasi, nisiufikishe ujumbe na nisitoe ushauri mzuri kwenu? Hapo hamtaniongezea isipokuwa upotevu na kuwa mbali na wema».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net