Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 62

Hud 11:62

هود

قَالُوا۟ يَـٰصَـٰلِحُ قَدْ كُنتَ فِينَا مَرْجُوًّا قَبْلَ هَـٰذَآ ۖ أَتَنْهَىٰنَآ أَن نَّعْبُدَ مَا يَعْبُدُ ءَابَآؤُنَا وَإِنَّنَا لَفِى شَكٍّ مِّمَّا تَدْعُونَآ إِلَيْهِ مُرِيبٍ

Maana

Wakasema: Ewe Saleh! Hakika kabla ya haya ulikuwa unatarajiwa heri kwetu. Je, unatukataza kuwaabudu wale ambao baba zetu walikuwa wakiwaabudu? Na hakika sisi tuna shaka na wasiwasi kwa hayo unayotuitia.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wakasema: Ewe Swaleh! Hakika kabla ya haya ulikuwa unatarajiwa kheri kwetu. Je, unatukataza tusiwaabudu waliyo kuwa wakiwaabudu baba zetu? Na hakika sisi tuna shaka na wasiwasi kwa hayo unayo tuitia. [62]

[62] Wakasema: Ewe Swaleh! Hakika wewe ulikuwa kwetu mtu wa kutarajiwa mema, na kupendwa, na kutukuzwa katika nyoyo zetu, kabla ya haya unayo tuitia! Hivyo unatutaka tuache ibada waliyo kuwa wakiabudu baba zetu na tuliyo izoea sisi na wao? Hakika sisi tuna shaka na huo wito wako wa kumuabudu Mwenyezi Mungu Mmoja. Haya ni mambo ya kukutilia shaka na dhana mbovu wewe na huo wito wako!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Thamûd wakasema kumwambia Ṣãlîḥ, «Kwa hakika, kabla ya neno hili ulilotwambia, tulikuwa tuna matumaini kwamba utakuwa ni kiongozi mwenye kusikilizwa,. Je, unatukataza kuwaabudu waungu ambao baba zetu walikuwa wakiwaabudu? Hakika sisi tuko kwenye shaka yenye kutia wasiwasi juu ya mwito wako wa kutuita sisi tumuabudu Allah Mtukufu Peke Yake».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net