Hud 11:61
هودوَإِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَـٰلِحًا ۚ قَالَ يَـٰقَوْمِ ٱعْبُدُوا۟ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُۥ ۖ هُوَ أَنشَأَكُم مِّنَ ٱلْأَرْضِ وَٱسْتَعْمَرَكُمْ فِيهَا فَٱسْتَغْفِرُوهُ ثُمَّ تُوبُوٓا۟ إِلَيْهِ ۚ إِنَّ رَبِّى قَرِيبٌ مُّجِيبٌ
Na kina Thamud tuliwatumia ndugu yao Saleh. Akasema: Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna mungu yeyote isipokuwa Yeye. Yeye ndiye aliyewaumba kutoka katika ardhi, na akawaweka humo imara. Basi mwombeni msamaha, kisha mtubu kwake. Hakika Mola wangu Mlezi yupo karibu, anaitikia maombi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kina Thamud tuliwapelekea ndugu yao Swaleh. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Yeye ndiye aliye kuumbeni katika ardhi, na akakuwekeni humo. Basi mwombeni msamaha, kisha mtubu kwake. Hakika Mola wangu Mlezi yupo karibu, anaitikia maombi. [61]
[61] Na kwa kina Thamud tulimtuma mmoja wao ambaye amefungana nao kwa nasaba na mapenzi, naye ni Swaleh. Akawaambia: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu pekee. Nyinyi hamna anaye stahiki kuabudiwa isipo kuwa Yeye. Yeye ndiye aliye kuumbeni kwenye ardhi, na akakuwekeni muiimarishe, na muitoe mavuno ya kukufaeni kheri yake...Basi mwombeni Yeye apate kukusameheni makosa yenu yaliyo kwisha tangulia. Kisha mrejee kwake na majuto kwa mlivyo muasi, na mkubali kumtii, kila mnapo tumbukia katika madhambi. Hakika Mola wangu Mlezi yupo karibu kwa rehema, na Mwenye kupokea maombi kwa mwenye kutaka msamaha na kumwomba. Tazama maelezo ya ki-ilimu juu ya Aya 73 katika Sura Al-Aa'raaf (7).
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tulimtuma kwenda kwa Thamûd ndugu yao Ṣãliḥ akasema kuwaambia, «Enyi watu wangu, muabuduni Allah Mtukufu, Peke Yake. hamna mungu yoyote anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu. Basi mtakasieni ibada. Yeye Ndiye Aliyeanza kuwaumba kutokamana na ardhi, kwa kumuumba baba yenu Ãdam kutokamana na hiyo, na akawafanya nyinyi ni wenye kuiimarisha. Hivyo basi, muombeni Awasamehe madhambi yenu, na rudini Kwake kwa kutubia kidhati. Hakika Mola wangu yuko karibu na yule anayemtakasia ibada na akawa na hamu ya kuja Kwake kwa kutubia, ni Mwenye kumuitikia anapomuomba».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net