Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 60

Hud 11:60

هود

وَأُتْبِعُوا۟ فِى هَـٰذِهِ ٱلدُّنْيَا لَعْنَةً وَيَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۗ أَلَآ إِنَّ عَادًا كَفَرُوا۟ رَبَّهُمْ ۗ أَلَا بُعْدًا لِّعَادٍ قَوْمِ هُودٍ

Maana

Na wakafuatishiwa laana katika dunia hii na Siku ya Kiyama. Basi tambueni mtanabahi kuwa hakika kina 'Aadi walimkufuru Mola wao Mlezi. Na tambueni mtanabahi kuwa hakika waliangamizwa kina 'Aadi, kaumu ya Hud.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wakafuatishiwa laana katika dunia hii na Siku ya Kiyama. Basi tambueni mtanabahi! Hakika kina A'adi walimkufuru Mola wao Mlezi. Na tambueni mtanabahi kuwa hakika waliangamizwa kina A'adi, kaumu ya Huud. [60]

[60] Kwa hivyo wakastahiki kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na Malaika, na watu wote kupata laana ya hapa duniani, na laana ya kuwafuatia Siku ya Kiyama. Basi na atanabahi kila mwenye kuijua khabari ya A'adi kwamba hao kina A'adi waliikataa neema ya Muumba wao kwao, wala hawakuishukuru kwa kumuamini Yeye peke yake. Kwa hivyo ndio wakawa wanastahili wafukuzwe kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu, na wateremshiwe maangamizo makali! Hebu zingatieni maangamizo yao kwa kumkadhibisha Huud!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wakafuatiwa, katika ulimwengu huu, na laana ya Allah Mtukufu, na wakafuatwa na hasira Zake Siku ya Kiyama. Jueni mtanabahi kwamba ‛Ãd walimkanusha Mola wao na wakawakanusha Mitume Wake. Jueni mtanabahi kwamba umbali na rehema za Allah Mtukufu na maangamivu yatawashukia ‛Ãd, watu wa Hûd, kwa sababu ya ushirikina wao na kukanusha kwao neema ya Mola wao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net