Hud 11:59
هودوَتِلْكَ عَادٌ ۖ جَحَدُوا۟ بِـَٔايَـٰتِ رَبِّهِمْ وَعَصَوْا۟ رُسُلَهُۥ وَٱتَّبَعُوٓا۟ أَمْرَ كُلِّ جَبَّارٍ عَنِيدٍ
Na hao ndio kina 'Aadi. Walizikufuru Ishara za Mola wao Mlezi, na wakawaasi Mitume wake, na wakafuata amri ya kila jabari mkaidi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hao ndio kina A'adi. Walizikanusha Ishara za Mola wao Mlezi, na wakawaasi Mitume wake, na wakafuata amri ya kila jabari mwenye inda. [59]
[59] Hao, basi, ndio kina A'adi! Walizikataa hoja zote zilizo wazi, na wakawaasi Mitume wote wa Mwenyezi Mungu, kwa vile kumuasi yule Mtume wao aliye tumwa kwao, na vile kumt'ii kila aliye kuwa jeuri na mwingi wa inda katika maraisi wao na wakubwa wao!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hao ndio‛Ãd, walikanusha aya za Allah Mtukufu, wakaasi Mitume Wake na wakatii amri ya kila anayemfanyia kiburi Allah Mtukufu asiyekubali haki wala kuinyoshea shingo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net