Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 58

Hud 11:58

هود

وَلَمَّا جَآءَ أَمْرُنَا نَجَّيْنَا هُودًا وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مَعَهُۥ بِرَحْمَةٍ مِّنَّا وَنَجَّيْنَـٰهُم مِّنْ عَذَابٍ غَلِيظٍ

Maana

Na ilipofika amri yetu, tulimwokoa Hud na wale walioamini pamoja naye, kwa rehema itokayo kwetu. Na tukawaokoa kutokana na adhabu nzito.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ilipo fika amri yetu, tulimwokoa Huud na walio amini pamoja naye, kwa rehema itokayo kwetu. Na tukawaokoa na adhabu ngumu. [58]

[58] Na ilipo kuja amri yetu ya kuwahiliki qaumu ya A'adi tulimwokoa Hud, na walio amini pamoja naye, kutokana na adhabu ya upepo mkali ulio wahiliki, na tukawaokoa na adhabu kubwa ya duniani na Akhera. Na hayo ni kwa sababu ya rehema yetu juu yao, kwa kuwawezesha kushika Imani.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na ilipokuja amri yetu kuwaadhibu watu wa Hûd, tulimuokoa Hûd na Waumini miongoni mwao kwa wema wetu juu yao na huruma, na tukawaokoa wao na adhabu kali Aliyoishukisha Allah Mtukufu kwa hao ‛Ãd, wakapambaukiwa na huku hakuna kionekanacho isipokuwa makazi yao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net