Hud 11:57
هودفَإِن تَوَلَّوْا۟ فَقَدْ أَبْلَغْتُكُم مَّآ أُرْسِلْتُ بِهِۦٓ إِلَيْكُمْ ۚ وَيَسْتَخْلِفُ رَبِّى قَوْمًا غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّونَهُۥ شَيْـًٔا ۚ إِنَّ رَبِّى عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ حَفِيظٌ
Na wakikengeuka, "Basi hakika mimi nimekwishawafikishia yale niliyotumwa nayo kwenu. Na Mola wangu Mlezi atawaleta watu wengine badala yenu, wala nyinyi hamumdhuru kitu Yeye. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kuhifadhi vyema kila kitu."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ikiwa watarudi nyuma, basi mimi nimekwisha kufikishieni niliyo tumwa kwenu. Na Mola wangu Mlezi atawaleta watu wengine badala yenu, wala nyinyi hamumdhuru kitu Yeye. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kuhifadhi kila kitu. [57]
[57] Na mkiukataa wito wangu, basi kukataa kwenu hakunidhuru kitu. Na mwisho mbaya utakuwa wenu. Kwani mimi nimekwisha kufikishieni ujumbe aliyo nituma Mwenyezi Mungu kwenu. Na sina jukumu ila kufikisha tu. Na Mwenyezi Mungu atakuangamizeni nyinyi, na awalete watu wengine wachukue majumba yenu na mali yenu! Na nyinyi hamumdhuru kitu chochote Yeye kwa kukataa kwenu kumuabudu! Hakika Mola wangu Mlezi ni Mlinzi wa kila kitu, Mwenye kujua kila kitu. Basi hapana katika mtendalo linalo fichikana kwake, wala haghafiliki kukutieni nguvuni.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mkiyapa mgongo yale ninayowalingania kwayo ya kumpwekesha Allah Mtukufu na kumtakasia ibada, basi nimeshaufikisha ujumbe wa Mola wangu kwenu na hoja ishasimama kwenu nyinyi, na Allah Mtukufu atawaangamiza kwa kuwa hamkumuamini, na Atawaleta watu wengine ambao watashika nafasi zenu katika majumba yenu na mali yenu, na ambao watamtakasia Allah Mtukufu ibada. Na nyinyi hamtamdhuru Yeye kitu chochote. Hakika Mola wangu amekidhibiti kila kitu na kukihifadhi; Yeye Ndiye Mwenye kunitunza msinifanyie ubaya.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net