Hud 11:56
هودإِنِّى تَوَكَّلْتُ عَلَى ٱللَّهِ رَبِّى وَرَبِّكُم ۚ مَّا مِن دَآبَّةٍ إِلَّا هُوَ ءَاخِذٌۢ بِنَاصِيَتِهَآ ۚ إِنَّ رَبِّى عَلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ
Hakika mimi nimemtegemea Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Hakuna kiumbe yeyote isipokuwa Yeye anamwendesha atakavyo. Hakika Mola wangu Mlezi yuko kwenye njia iliyonyooka."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika mimi nimemtegemea Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wangu na Mola Mlezi wenu. Hapana kiumbe yeyote ila Yeye anamwendesha atakavyo. Hakika Mola wangu Mlezi yuko juu ya Njia Iliyo Nyooka. [56]
[56] Mimi namtegemea Mwenyezi Mungu. Na Yeye ndiye Mwenye mamlaka juu ya mambo yangu na mambo yenu. Wala hashindwi na kitu chochote katika kupinga vitimbi vyenu. Na Yeye ni Muweza wa kila kitu. Basi hapana kiumbe yoyote ila yuko chini ya madaraka yake, na Yeye ndiye Mwenye kumsarifu atakavyo. Basi Yeye hashindwi na kunilinda na maudhi yenu, wala hashindwi kukuangamizeni! Hapana shaka vitendo vya Mola wangu Mlezi vinafuata njia ya Haki na Uadilifu katika ufalme wake. Yeye huwanusuru Waumini watendao mema, na huwahizi makafiri waharibifu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mimi nimetegemea kwa Allah Mtukufu, Mola wangu na Mola wenu, Mmiliki wa kila kitu na Mwenye kukiendesha. Hakuna kitu chenye kunipata isipokuwa kwa amri Yake. Na Yeye Ndiye Muweza wa kila kitu. Hakuna kitu chochote kinachotambaa kwenye ardhi hii isipokuwa Allah Mtukufu Amekimiliki na kiko chini ya mamlaka Yake na uendeshaji Wake. Hakika Mola wangu Yuko kwenye njia iliyolingana sawa, kwa maana kwamba ni muadilifu katika hukumu Zake, sheria Zake na amri Zake, Anamlipa mwema kwa wema Wake na muovu kwa uovu wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net