Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 55

Hud 11:55

هود

مِن دُونِهِۦ ۖ فَكِيدُونِى جَمِيعًا ثُمَّ لَا تُنظِرُونِ

Maana

Badala ya Yeye. Basi nyinyi nyote nipangieni njama, na kisha msinipe muhula!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mkamwacha Yeye. Basi nyote nyinyi nipangieni vitimbi, na kisha msinipe muhula! [55]

[55] Wala mimi sikujalini, wala siwajali miungu yenu hiyo ambayo mnadai kuwa imenipatiliza kwa uovu! Basi saidianeni, nyinyi na miungu yenu, kunifanyia vitimbi. Kisha wala msiakhirishe hiyo adhabu yenu kwangu hata dakika moja, kama mnaweza!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

badala ya Allah Mtukufu, miongoni mwa wale wafananishwao na Yeye na masanamu. Basi angalieni na mfanye bidii, nyinyi na hao mnaodai kati ya waungu wenu, kunipatia madhara, kisha msilicheleweshe hilo hata kitambo kidogo kiasi cha kupepesa jicho. Hivyo ni kwamba Hûd ana imani thabiti kwamba hayatampata yeye kutoka kwao wala kutoka kwa waungu wao madhara yoyote.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net