Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 54

Hud 11:54

هود

إِن نَّقُولُ إِلَّا ٱعْتَرَىٰكَ بَعْضُ ءَالِهَتِنَا بِسُوٓءٍ ۗ قَالَ إِنِّىٓ أُشْهِدُ ٱللَّهَ وَٱشْهَدُوٓا۟ أَنِّى بَرِىٓءٌ مِّمَّا تُشْرِكُونَ

Maana

Sisi tunasema: ʻBaadhi ya miungu yetu imekusibu kwa baa.ʼˮ Akasema, “Hakika, mimi ninamshuhudisha Mwenyezi Mungu, na nyinyi shuhudieni, ya kwamba mimi niko mbali na hao mnaowafanya washirika.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sisi tunasema: Baadhi katika miungu yetu imekusibu kwa baa. Akasema: Hakika mimi namshuhudisha Mwenyezi Mungu, na nyinyi shuhudieni, ya kwamba mimi najitenga mbali na hao mnao wafanya washirika, [54]

[54] Na hatuna la kusema juu ya msimamo wako nasi ila kuwa mmojapo katika miungu yetu imekupatiliza kwa shari, ndio maana ukawa unaropokwa maneno haya! Naye akasema naye ameshikilia Imani yake na anawapinga: Ninasema, na namshuhudisha Mwenyezi Mungu kwa haya niyasemayo, na nakushuhudisheni nyinyi, ya kwamba mimi najitenga mbali kabisa na maradhi ya ushirikina mliyo nayo. Kwani nyinyi ni wagonjwa!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

«Sisi hatusemi isipokuwa kwamba baadhi ya waungu wetu wamekutia wazimu kwa sababu ya kukataza kwako wasiabudiwe.» Akawaambia, «Mimi namshuhudisha Allah Mtukufu haya ninayoyasema na nawashudisha nyinyi kwamba mimi niko mbali na vile mnavyovishirikisha».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net