Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 53

Hud 11:53

هود

قَالُوا۟ يَـٰهُودُ مَا جِئْتَنَا بِبَيِّنَةٍ وَمَا نَحْنُ بِتَارِكِىٓ ءَالِهَتِنَا عَن قَوْلِكَ وَمَا نَحْنُ لَكَ بِمُؤْمِنِينَ

Maana

Wakasema, "Ewe Hud! Hujatuletea ushahidi ulio wazi. Wala sisi hatuiachi miungu yetu kwa kufuata kauli yako. Na wala sisi hatukuamini wewe.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wakasema: Ewe Huud! Hujatuletea dalili wazi. Wala sisi hatuiachi miungu yetu kwa kufuata kauli yako. Na wala sisi hatukuamini wewe. [53]

[53] Wakasema: Ewe Huud! Hukutuletea hoja yoyote iliyo wazi ya kuonyesha ukweli wa hayo unayo tuitia. Wala sisi hatutoacha kuabudu miungu yetu kwa kufuata kauli yako tu! Je, tuwawache hao, na hali sisi hatukusadiki wewe?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wakasema, «Ewe Hûd, hukutujia na hoja zilizo wazi juu ya usahihi wa yale unayotuitia. Na sisi si wenye kuwaacha waungu wetu tunaowaabudu kwa sababu ya maneno yako. Na sisi si wenye kukuamini wewe katika hilo unalolidai».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net