Hud 11:52
هودوَيَـٰقَوْمِ ٱسْتَغْفِرُوا۟ رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوٓا۟ إِلَيْهِ يُرْسِلِ ٱلسَّمَآءَ عَلَيْكُم مِّدْرَارًا وَيَزِدْكُمْ قُوَّةً إِلَىٰ قُوَّتِكُمْ وَلَا تَتَوَلَّوْا۟ مُجْرِمِينَ
Na enyi kaumu yangu! Mwombeni msamaha Mola wenu Mlezi, kisha mtubie kwake. Atawatumia mbingu zenye kunyesha mvua ya kumiminika kwa wingi, na atawazidishia nguvu juu ya nguvu zenu. Wala msigeuke mkawa wahalifu."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na enyi watu wangu! Muombeni msamaha Mola wenu Mlezi, kisha mtubie kwake. Atakuleteeni mbingu zenye kunyesha mvua ya kumiminika, na atakuzidishieni nguvu juu ya nguvu zenu. Wala msigeuke mkawa wakosefu. [52]
[52] Enyi watu! Mtakeni aliye kuumbeni akusameheni madhambi yaliyo kwisha tangulia. Kisha rejeeni kwake. Hapana shaka mkifanya hayo atakuleteeni mvua nyingi mfululizo, basi zitaongezeka kheri zenu, na zitazidi nguvu zenu juu ya nguvu mnazo jivunia sasa! Wala msiyawache haya ninayo kuiteni muyafwate, mkashikilia maasi ambayo yatakuangamizeni kwenye hilaki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
«Enyi watu wangu, takeni msamaha wa Allah Mtukufu kwa kumuamini Yeye, kisha mtubie Kwake kutokana na dhambi zenu. Kwani nyinyi mkifanya hivyo, Atawateremshia mvua yenye kufuatana iliyo nyingi, hivyo basi mazuri yenu yatakuwa mengi na Atawaongezea nguvu juu ya nguvu mlizonazo kwa wingi wa watoto wenu na mfuatano wa neema juu yenu. Na msiyape mgongo yale ninayowalingania nyinyi kwayo mkawa ni wenye kuendelea juu ya makosa yenu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net