Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 51

Hud 11:51

هود

يَـٰقَوْمِ لَآ أَسْـَٔلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا ۖ إِنْ أَجْرِىَ إِلَّا عَلَى ٱلَّذِى فَطَرَنِىٓ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ

Maana

Enyi watu wangu! Siwaombi ujira kwa ajili ya haya. Ujira wangu hauko isipokuwa kwa Yule aliyeniumba. Basi hamtumii akili?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi watu wangu! Sikuombeni ujira kwa ajili ya haya. Haukuwa ujira wangu ila kwa Yule aliye niumba. Basi hamtumii akili? [51]

[51] Enyi watu! Kwa nasaha hii sitaki kwenu kulipwa kwa cheo, au utawala, au mali. Kwani ujira wangu uko kwa Mwenyezi Mungu aliye niumba. Wala haikufaliini nyinyi mkawa mmechotwa akili zenu kwa kughafilika msitambue linalo kufaeni na linalo kudhuruni!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi watu wangu, mimi siwaombi malipo yoyote, kwa haya niwalinganiyayo ya kumtakasia Allah Mtukufu ibada na kuacha kuabudu masanamu,. Malipo yangu mimi ya kuwalingania nyinyi hayako juu ya yoyote isipokuwa Allah Mtukufu aliyeniumba. Basi hamtii akili mkatenganisha baina ya ukweli na upotofu?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net