Hud 11:50
هودوَإِلَىٰ عَادٍ أَخَاهُمْ هُودًا ۚ قَالَ يَـٰقَوْمِ ٱعْبُدُوا۟ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُۥٓ ۖ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا مُفْتَرُونَ
Na kwa kina 'Aadi tulimtuma ndugu yao Hud. Akasema, "Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu! Hamna mungu isipokuwa Yeye tu. Nyinyi si chochote isipokuwa ni wazushi tu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kwa kina A'adi tulimtuma ndugu yao Hud. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu! Nyinyi hamna mungu isipo kuwa Yeye. Nyinyi si chochote ila ni wazushi tu. [50]
[50] Na Sisi tuliwapelekea Kaumu ya A'adi wa mwanzo ndugu yao katika kabila yao, naye ni huyo Huud. Akawaambia: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu pekee. Kwani hamna anaye stahiki kuabudiwa isipo kuwa Yeye. Na nyinyi si cho chote ila mnazua uwongo tu kudai kuwa Mwenyezi Mungu ana washirika wanao stahiki nao kuabudiwa ili wawe waombezi wenu kwa Mwenyezi Mungu! Tazama maelezo ya ki-ilimu juu ya Aya 65 katika Sura Al-Aa'raaf. (7).
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tuliwamtumia watu wa kabila la ‛Ăd ndugu yao Hûd. Alisema kuwaambia, «Enyi watu wangu, muabuduni Allah Mtukufu, Peke Yake. Nyinyi hamna mungu anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye. Basi mtakasieni Yeye ibada. Kwani nyinyi hamkuwa, katika kumshirikisha kwenu Allah Mtukufu, isipokuwa ni warongo».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net