Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 49

Hud 11:49

هود

تِلْكَ مِنْ أَنۢبَآءِ ٱلْغَيْبِ نُوحِيهَآ إِلَيْكَ ۖ مَا كُنتَ تَعْلَمُهَآ أَنتَ وَلَا قَوْمُكَ مِن قَبْلِ هَـٰذَا ۖ فَٱصْبِرْ ۖ إِنَّ ٱلْعَـٰقِبَةَ لِلْمُتَّقِينَ

Maana

Hizi ni katika habari za ghaibu tunazokufunulia. Hukuwa ukizijua wewe, wala kaumu yako, kabla ya haya. Basi subiri! Hakika Mwisho mwema ni wa wacha Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hizi ni katika khabari za ghaibu tunazo kufunulia. Hukuwa ukizijua wewe, wala watu wako, kabla ya hii. Basi subiri! Hakika Mwisho ni wa wachamngu. [49]

[49] Hizo ni simulizi tulizo kusimulia wewe, ewe Nabii, juu ya Nuhu na kaumu yake. Hizo ni khabari za ghaibu ambazo hazijui ila Mwenyezi Mungu. Wewe wala watu wako hamkuwa mkizijua kwa namna hii, na kwa tafsili hii, kabla ya wahyi huu. Basi wewe vumilia maudhi ya watu wako, kama walivyo subiri Manabii wa kabla yako. Kwani mwisho wako ni kufuzu kama ulivyo kuwa mwisho wao hao. Na Mwisho mwema daima ni wa wale wanao iogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kuamini na kutenda vitendo vyema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Habari hiyo tuliyokuhadithia kuhusu Nûḥ na watu wake ni miongoni mwa habari za ghaibu zilizopita, ambazo tunakuletea wahyi juu yake, hukuwa ukizijua, wewe wala watu wako, kabla ya maelezo haya. Basi subiri juu ya ukanushaji wa watu wako na makero yao wanayokufanyia kama walivyosubiri Manabii huko nyuma. Na mwisho mwema wa duniani na Akhera ni wa waogopao wanaomcha Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net