Hud 11:48
هودقِيلَ يَـٰنُوحُ ٱهْبِطْ بِسَلَـٰمٍ مِّنَّا وَبَرَكَـٰتٍ عَلَيْكَ وَعَلَىٰٓ أُمَمٍ مِّمَّن مَّعَكَ ۚ وَأُمَمٌ سَنُمَتِّعُهُمْ ثُمَّ يَمَسُّهُم مِّنَّا عَذَابٌ أَلِيمٌ
Ikasemwa: Ewe Nuhu! Shuka kwa salama itokayo kwetu, na baraka nyingi juu yako na juu ya umma miongoni mwa wale walio pamoja nawe. Na zitakuwapo umma tutakazozistarehesha, na kisha zitaguswa na adhabu chungu itokayo kwetu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ikasemwa: Ewe Nuhu! Shuka kwa salama itokayo kwetu, na baraka nyingi juu yako na juu ya watu walio pamoja nawe. Na zitakuwapo kaumu tutakazo zistarehesha, na kisha zitashikwa na adhabu chungu itokayo kwetu. [48]
[48] Akaambiwa kwa wahyi: Ewe Nuhu! Teremka nchi kavu kutokana na hiyo Safina ya uwokovu, salama usalimina, kwa amani itokanayo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na baraka nyingi zitokazo kwa Mwenyezi Mungu juu yako na juu ya hao walio pamoja nawe, ambao watakuja kuwa mataifa mbali mbali baada yako. Na baadhi yao watapata baraka ya Imani na ut'iifu, na baadhi yao watakuwa watu wanao itaka starehe ya dunia, na watapata starehe yake bila ya kuit'ii Haki. Kisha Siku ya Kiyama itawapata adhabu chungu na kali.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Akasema, «Ewe Nûḥ, Shuka kwenye ardhi kavu kutoka kwenye jahazi, kwa amani na salama zitokazo kwetu, na baraka ikishuka juu yako na juu ya ummah katika wale walioko na wewe. Na kuna ummah na makundi miongoni mwa watu wa uovu ambao tutawastarehesha katika uhai wa kilimwengu mpaka ufike muda wao wa kuishi kisha iwapate wao kutoka kwetu adhabu iumizayo Siku ya Kiyama».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net