Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 47

Hud 11:47

هود

قَالَ رَبِّ إِنِّىٓ أَعُوذُ بِكَ أَنْ أَسْـَٔلَكَ مَا لَيْسَ لِى بِهِۦ عِلْمٌ ۖ وَإِلَّا تَغْفِرْ لِى وَتَرْحَمْنِىٓ أَكُن مِّنَ ٱلْخَـٰسِرِينَ

Maana

Nuhu akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Mimi najikinga kwako kutokana na kukuomba nisilo na elimu nalo. Na kama hunisamehi na ukanirehemu, nitakuwa katika waliohasiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Nuhu akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Mimi najikinga kwako nisikuombe nisio na ujuzi nalo. Na kama hunisamehe na ukanirehemu, nitakuwa katika walio khasiri. [47]

[47] Nuhu akasema: Ewe Muumba wangu, uliye tawala mambo yangu yote! Mimi nakuangukia Wewe. Sitakuomba nisicho kijua hakika yake. Nawe nisamehe kwa niliyo yasema kutokana na huruma zangu. Kama hukunipa fadhila ya msamaha wako, na ukanirehemu kwa rehema yako, nitakuwa katika makundi ya walio khasiri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Akasema Nûḥ, «Ewe Mola wangu, Mimi najihami kwako na nataka hifadhi kukuomba kitu nisiokuwa na ujuzi nacho, na usiponisamehe dhambi zangu na ukanihurumia kwa rehema zako, nitakuwa ni miongoni mwa wale waliojinyima hadhi zao na wakaangamia».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net