Hud 11:46
هودقَالَ يَـٰنُوحُ إِنَّهُۥ لَيْسَ مِنْ أَهْلِكَ ۖ إِنَّهُۥ عَمَلٌ غَيْرُ صَـٰلِحٍ ۖ فَلَا تَسْـَٔلْنِ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِۦ عِلْمٌ ۖ إِنِّىٓ أَعِظُكَ أَن تَكُونَ مِنَ ٱلْجَـٰهِلِينَ
Akasema: Ewe Nuhu! Huyu si katika ahali zako. Hakika yeye ni (wa) matendo yasiyo mema. Basi usiniombe jambo usilo na elimu nalo. Mimi nakuwaidhi usije ukawa miongoni mwa wajinga.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akasema: Ewe Nuhu! Huyu si katika ahali zako. Mwendo wake si mwema. Basi usiniombe jambo usio na ujuzi nalo. Mimi nakuwaidhi usije ukawa miongoni mwa wajinga. [46]
[46] Allah Subhanahu akasema: Hakika huyo mwanao si katika ahali zako. Kwani yeye kwa ukafiri wake na mwendo wake pamoja na makafiri amekata makhusiano baina yako na yeye. Naye ametenda vitendo visio vyema. Kwa hivyo amekuwa si katika wewe. Nawe usitake jambo usilo lijua, kuwa ndilo au silo. Wala usende kufuata huruma zako. Na mimi nakuongoza njia ya Haki ili usiwe katika wajinga ukasahau kwa huruma zako Hakika iliyo thibiti!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Akasema, «Ewe Nûḥ, hakika yule mtoto wako aliyeangamia si katika jamaa ambao nilikuahidi kuwa nitawaokoa. Hii ni kwa sababu ya ukafiri wake na kufanya kwake matendo yasiyokuwa mema. Na mimi nakukataza usiniombe jambo usiokuwa na ujuzi nalo. Mimi nakusihi usiwe ni miongoni mwa wajinga kwa kuniomba hilo».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net