Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 45

Hud 11:45

هود

وَنَادَىٰ نُوحٌ رَّبَّهُۥ فَقَالَ رَبِّ إِنَّ ٱبْنِى مِنْ أَهْلِى وَإِنَّ وَعْدَكَ ٱلْحَقُّ وَأَنتَ أَحْكَمُ ٱلْحَـٰكِمِينَ

Maana

Na Nuhu alimwomba Mola wake Mlezi: Ee Mola wangu Mlezi! Hakika mwanangu ni katika ahali zangu, na hakika ahadi yako ndiyo ya haki. Na Wewe ndiye hakimu bora zaidi ya wote wanaohukumu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Nuhu alimwomba Mola wake Mlezi: Ee Mola Mlezi wangu! Hakika mwanangu ni katika ahali zangu, na hakika ahadi yako ni haki. Na Wewe ni Mwenye haki kuliko mahakimu wote. [45]

[45] Huruma ilimshika Nuhu moyoni mwake kwa ajili ya mwanawe. Akamwomba Mola Mlezi wake kwa unyenyekevu na kuona huruma, akasema: Ewe Muumba wangu, uliye nianzisha nami sijawa chochote! Hakika huyu mwanangu ni kipande cha nafsi yangu, naye ni katika ahali zangu. Na Wewe umeahidi kuwa utawaokoa ahali zangu, na ahadi yako ni ya kweli, madhubuti, lazima iwe. Na hapana muadilifu kama Wewe! Kwani Wewe ndiye Mjuzi kushinda wote, na Wewe ni mwingi wa hikima kuliko wote wenye kuhukumu!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Nûḥ alimlingania Mola Wake kwa kumuomba na akasema, «Mola wangu, wewe umeniahidi kwamba utaniokoa, mimi na jamaa zangu, tusizame na tusiangamie, na hakika mtoto wangu ni miongoni mwa watu wa nyumbani kwangu, na ahadi yako ndio kweli ambayo haibadiliki, na wewe ndiye hodari zaidi wa wenye kuhukumu na muadilifu wao zaidi».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net