Hud 11:44
هودوَقِيلَ يَـٰٓأَرْضُ ٱبْلَعِى مَآءَكِ وَيَـٰسَمَآءُ أَقْلِعِى وَغِيضَ ٱلْمَآءُ وَقُضِىَ ٱلْأَمْرُ وَٱسْتَوَتْ عَلَى ٱلْجُودِىِّ ۖ وَقِيلَ بُعْدًا لِّلْقَوْمِ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Na ikasemwa: "Ewe ardhi! Meza maji yako. Na ewe mbingu! Jizuie." Basi maji yakadidimia chini, na amri hiyo ikapitishwa, na (jahazi) likasimama juu ya (mlima) wa Al-Juudiy. Na ikasemwa: Wapotelee mbali kaumu madhalimu!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ikasemwa: Ewe ardhi! Meza maji yako. Na Ewe mbingu! Jizuie. Basi maji yakadidimia chini, na amri ikapitishwa, na (jahazi) likasimama juu ya (mlima) wa Al Juudiy. Na ikasemwa: Wapotelee mbali watu walio dhulumu! [44]
[44] Walipo kwisha hiliki makafiri kwa kuzamishwa, ikaja amri ya Mwenyezi Mungu ya maumbile. Ikasemwa kwa hukumu ya uumbaji: Ewe ardhi! Yameze maji yako, na wewe mbingu! Sita na kuteremsha maji. Yakaondoka maji kwenye ardhi, wala kisiongezeke chochote kutoka mbinguni. Hukumu ya Mwenyezi Mungu ya kuhiliki ikamalizika. Jahazi likatua na likasimama juu ya mlima uitwao Al Juudiy. Na Mwenyezi Mungu akawahukumia walio dhulumu kwa kuwatenga na rehema yake. Ikasemwa: Wateketee kaumu walio dhulumu kwa sababu ya dhulma zao. Mlima huo uko Mosal (kaskazini mwa Iraq na kusini ya Turki) Ulikuwa maarufu hapo kale.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Akasema Allah Mtukufu kuiambia ardhi, baada ya watu wa Nûḥ kuangamia, «Ewe ardhi! Kunywa maji yako. Na ewe mbingu! Simamisha kunyesha mvua.» Na maji yakapungua na yakanywea, na amri ya Allah Mtukufu ikapitishwa ya kuangamia watu wa Nûḥ, na jahazi ikaegesha juu jabali la Jūdīy. Na hapo kukasemwa, «Kuwa mbali (na rehema za Allah Mtukufu) ni kwa wale madhalimu waliokiuka mipaka ya Allah Mtukufu na wasiamini».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net