Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 43

Hud 11:43

هود

قَالَ سَـَٔاوِىٓ إِلَىٰ جَبَلٍ يَعْصِمُنِى مِنَ ٱلْمَآءِ ۚ قَالَ لَا عَاصِمَ ٱلْيَوْمَ مِنْ أَمْرِ ٱللَّهِ إِلَّا مَن رَّحِمَ ۚ وَحَالَ بَيْنَهُمَا ٱلْمَوْجُ فَكَانَ مِنَ ٱلْمُغْرَقِينَ

Maana

Akasema: Nitakimbilia mlimani unilinde kutokana na maji. (Nuhu) akasema: "Leo hakuna wa kulindwa kutokana na amri ya Mwenyezi Mungu isipokuwa yule aliyemrehemu mwenyewe." Na wimbi likawatenganisha, basi akawa katika waliozama majini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Akasema: Nitakimbilia mlimani unilinde na maji. (Nuhu) akasema: Leo hapana wa kulindwa na amri ya Mwenyezi Mungu ila aliye mrehemu mwenyewe. Na wimbi likawatenganisha, akawa katika walio zama. [43]

[43] Mtoto hakumt'ii baba yake mwenye kumwonea huruma! Akasema: Nitakwenda pahala pa kunilinda na maji! Baba, mwenye kujua hukumu ya Mwenyezi Mungu kwa wenye kuasi, alisema: Ewe mwanangu! Hakipatikani cha kuzuia hukumu ya Mwenyezi Mungu ya kuwazamisha walio dhulumu! Basi yule kijana akapotea kwenye macho ya baba yake anaye mnasihi nyuma ya wimbi lilio panda juu; akawa pamoja na wakanushao, walio zama, walio teketea.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mtoto wa Nûḥ akasema, «Nitakimbilia kwenye jabali nijihifadhi na maji na hilo litanizuia na kuzama.» Nûḥ akamjibu, «Leo hakuna kitu chenye kuzuia amri ya Allah Mtukufu na hukumu Yake iliyoteremka kwa viumbe, ya gharika na maangamivu, isipokuwa yule aliyehurumiwa na Allah Mtukufu Aliyetukuka, basi amini na upande jahazini pamoja na sisi.» Hapo mawimbi makubwa yalitenganisha baina ya Nûḥ na mwanawe na akawa ni miongoni mwa waliogharikishwa wenye kuangamia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net