Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 36

Hud 11:36

هود

وَأُوحِىَ إِلَىٰ نُوحٍ أَنَّهُۥ لَن يُؤْمِنَ مِن قَوْمِكَ إِلَّا مَن قَدْ ءَامَنَ فَلَا تَبْتَئِسْ بِمَا كَانُوا۟ يَفْعَلُونَ

Maana

Na akafunuliwa Nuhu akaambiwa, "Hataamini yeyote katika kaumu yako isipokuwa wale waliokwishaamini. Basi usisikitike kwa yale waliyokuwa wakiyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na akafunuliwa Nuhu akaambiwa: Hataamini yeyote katika watu wako ila wale walio kwisha amini. Basi usisikitike kwa waliyo kuwa wakiyatenda. [36]

[36] Mwenyezi Mungu akamletea wahyi Nuhu akamwambia: Hatakusadiki wala hataifuata Haki yeyote katika kaumu yako baada ya sasa, isipo kuwa wale walio kwisha tangulia kukuamini kabla ya hayo. Basi ewe Nuhu! Usihuzunike kwa sababu ya waliyo kuwa wakikutendea, ya kukukadhibisha, na kukuudhi. Kwani Sisi tutawalipiza karibu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Allah Mtukufu, Aliyetakasika na sifa za upungufu na kutukuka, Alimletea wahyi Nûh, amani imshukie, ilipolazimika adhabu juu ya watu wake kwamba hawatamuamini Allah Mtukufu isipokuwa walioamini kabla ya hapo, «basi usisikitike, ewe Nûh, juu ya yale waliokuwa wakiyafanya».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net