Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 35

Hud 11:35

هود

أَمْ يَقُولُونَ ٱفْتَرَىٰهُ ۖ قُلْ إِنِ ٱفْتَرَيْتُهُۥ فَعَلَىَّ إِجْرَامِى وَأَنَا۠ بَرِىٓءٌ مِّمَّا تُجْرِمُونَ

Maana

Au ndio wanasema, "Ameizua?" Sema, "Ikiwa nimeizua, basi kosa hilo ni juu yangu, na mimi niko mbali sana na makosa myatendayo."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Au ndio wanasema: Ameizua? Sema: Ikiwa nimeizua, basi kosa hilo ni juu yangu, na mimi sikhusiki na makosa myatendayo. [35]

[35] Nini msimamo wa washirikina kukhusu hadithi hizi za kweli? Watasema kazizua? Wakisema hivyo, basi waambie: Ikiwa nimezizua kama mnavyo dai, basi hilo ni kosa kubwa; ni juu yangu mimi tu dhambi zake! Na ikiwa nimesema kweli, basi nyinyi ndio wenye makosa, na mimi sikhusiki na matokeo ya makosa yenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Au je, wanasema hawa washirikina miongoni mwa watu wa Nûh, kwamba Nûh, amezua neno hili? Waambie, Nikiwa nimemzulia urongo Allah Mtukufu hilo, basi ni juu yangu mimi, peke yangu, dhambi ya hilo; na nikiwa ni mkweli, basi nyinyi ndio wahalifu wenye dhambi, na mimi niko mbali na ukafiri wenu, ukanushaji wenu na uhalifu wenu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net