Hud 11:34
هودوَلَا يَنفَعُكُمْ نُصْحِىٓ إِنْ أَرَدتُّ أَنْ أَنصَحَ لَكُمْ إِن كَانَ ٱللَّهُ يُرِيدُ أَن يُغْوِيَكُمْ ۚ هُوَ رَبُّكُمْ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ
Wala nasaha yangu haitawafaa kitu nikitaka kuwanasihi, ikiwa Mwenyezi Mungu anataka kuwapoteza. Yeye ndiye Mola wenu Mlezi, na kwake mtarejeshwa."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala nasaha yangu haikufaini kitu nikitaka kukunasihini, ikiwa Mwenyezi Mungu anataka kukuachieni mpotee. Yeye ndiye Mola wenu Mlezi; na kwake mtarejeshwa. [34]
[34] Wala nasaha yangu haitakufaeni kitu kwa kuwa tu nakutakieni kheri, ikiwa Mwenyezi Mungu anakutakeni mpotee kwa mujibu wa ilimu yake na uwezo wake kwa kuharibika nyoyo zenu, hata zimekuwa haziikubali Haki! Yeye Subhanahu ndiye Mola wenu Mlezi, naye atakurejesheni kwake Siku ya Kiyama. Na atakulipeni kwa mlivyo kuwa mkitenda.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
«Na hautawanufaisha nyinyi ushauri wangu na bidii yangu katika kuwalingania kwenye Imani, iwapo Allah Mtukufu Anataka kuwapoteza na kuwaangamiza. Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye mwenye kuwamiliki, na Kwake Yeye mtarejeshwa kesho Akhera kwa kuhesabiwa na kulipwa».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net