Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 33

Hud 11:33

هود

قَالَ إِنَّمَا يَأْتِيكُم بِهِ ٱللَّهُ إِن شَآءَ وَمَآ أَنتُم بِمُعْجِزِينَ

Maana

Akasema, "Hakika Mwenyezi Mungu tu ndiye atakayewaletea akitaka. Wala nyinyi si wenye kumshinda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Akasema (Nuhu) : Mwenyezi Mungu atakuleteeni akipenda, wala nyinyi siwenye kumshinda. [33]

[33] Nuhu akasema: Mambo haya yamo mikononi mwa Mwenyezi Mungu pekee. Yeye ndiye atakuleteeni alitakalo kwa hikima yake. Wala nyinyi hamwezi kuikimbia adhabu yake itakapo kuja. Kwani Yeye, Subhanahu, haemewi na chochote katika ardhi wala katika mbingu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Nûh, akasema kuwaambia watu wake, «Allah Mtukufu, Peke Yake, Ndiye Atakayewaletea nyinyi adhabu atakapo, na nyinyi si wenye kuiponyoka Akitaka kuwaadhibu, kwani Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, hakuna chochote chenye kumlemea katika ardhi wala katika mbingu».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net