Hud 11:37
هودوَٱصْنَعِ ٱلْفُلْكَ بِأَعْيُنِنَا وَوَحْيِنَا وَلَا تُخَـٰطِبْنِى فِى ٱلَّذِينَ ظَلَمُوٓا۟ ۚ إِنَّهُم مُّغْرَقُونَ
Na unda jahazi mbele ya macho yetu na kwa mujibu wa ufunuo wetu. Wala usiniongeleshe kuwatetea wale waliodhulumu. Kwani hao bila ya shaka watazamishwa."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na unda jahazi mbele ya macho yetu na kwa mujibu wa ufunuo wetu. Wala usinisemeze kuwatetea walio dhulumu. Kwani hao bila ya shaka watazamishwa. [37]
[37] Tukamwambia: Tengeneza chombo chini ya uangalizi na ulinzi wetu, wala usinisemeze kwa ajili ya hawa madhaalimu, kwa sababu nilikwisha itikia ombi lako, na nimekwisha amrisha wateketezwe kwa kuzamishwa. Tazama Aya 27 Surat Al Muuminun (23).
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
«Na utengeneze jahazi kwa maangalizi yetu na kwa amri yetu na msaada wetu, hali ya kuwa wewe uko kwenye utunzi wetu na hifadhi yetu, na usitake kwangu kuwapa muhula hawa waliojidhulumu nafsi zao, miongoni mwa watu wako, kwa ukafiri wao, kwani wao ni wenye kuzamishwa kwa mafuriko.» Katika hii aya pana kuthibitisha sifa ya ‛ayn (jicho ) kwa Allah Mtukufu Aliyetukuka kwa namna inavyonasibiana na Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net