Hud 11:30
هودوَيَـٰقَوْمِ مَن يَنصُرُنِى مِنَ ٱللَّهِ إِن طَرَدتُّهُمْ ۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ
Na enyi kaumu yangu! Ni nani atakayeninusuru kwa Mwenyezi Mungu nikiwafukuza hawa? Basi je, hamkumbuki?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na enyi watu wangu! Ni nani atakaye nisaidia kwa Mwenyezi Mungu nikiwafukuza hawa? Basi je, hamfikiri? [30]
[30] Enyi watu! Hapana yeyote awezaye kunikinga na adhabu ya Mwenyezi Mungu nikiwafukuza hao hali nao ni wenye kumuamini Yeye. Je, bado mngali mnashikilia ujinga wenu? Hamkumbuki basi kuwa hawa watu wanaye Mola wao Mlezi wa kuwalipia?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
«Na enyi watu wangu, ni nani mwenye kunizuia mimi na Allah Mtukufu Akinitesa kwa kuwafukuza kwangu Waumini? Kwani hamyazingatii mambo mkayajua yenye nafuu zaidi kwenu na yenye kufaa zaidi?»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net