Hud 11:29
هودوَيَـٰقَوْمِ لَآ أَسْـَٔلُكُمْ عَلَيْهِ مَالًا ۖ إِنْ أَجْرِىَ إِلَّا عَلَى ٱللَّهِ ۚ وَمَآ أَنَا۠ بِطَارِدِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ ۚ إِنَّهُم مُّلَـٰقُوا۟ رَبِّهِمْ وَلَـٰكِنِّىٓ أَرَىٰكُمْ قَوْمًا تَجْهَلُونَ
Na enyi kaumu yangu! Mimi siwaombi mali kwa ajili ya haya. Mimi sina ujira isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu; na mimi sitawafukuza walioamini. Hakika wao watakutana na Mola wao Mlezi, lakini mimi nawaona mnafanya ujinga.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na enyi watu wangu! Mimi sikuombeni mali kwa ajili ya haya. Mimi sina ujira ila kwa Mwenyezi Mungu; na mimi sitawafukuza walio amini. Hakika wao watakutana na Mola wao Mlezi, lakini mimi nakuoneni mnafanya ujinga. [29]
[29] Enyi watu! Mimi sitaki mali kwa kufikisha Ujumbe wa Mola wangu Mlezi, bali nataraji malipo yangu kwa Mwenyezi Mungu. Wala mimi siwafukuzi kwenye baraza yangu na kuingiana nami walio muamini Mola wao Mlezi, kwa sababu ya kuwa nyinyi mnawadharau tu! Kwani wao watakuja kukutana na Mola wao Mlezi Siku ya Kiyama na watanishitaki kwake ikiwa nimewafukuza kwa ajili ya ufakiri wao. Lakini mimi nakuoneni nyinyi ni watu msio jua nini kinacho watukuza viumbe mbele ya Mwenyezi Mungu! Ni utajiri na cheo kama mnavyo dai, au kufuata Haki na kufanya kheri?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Nûḥ, amani imshukie, akaendelea kuwaambia watu wake, «Enyi watu wangu, siwaombi kwa kuwaita nyinyi kumpwekesha Allah Mtukufu, mnipatie mali baada ya kuamini kwenu, kwani malipo ya ushauri wangu kwenu yako kwa Allah Mtukufu Peke Yake. Na si shughuli yangu mimi kuwafukuza Waumini, kwani wao ni wenye kukutana na Mola wao Siku ya Kiyama. Lakini mimi nawaona nyinyi kuwa ni watu msiojua, kwa kuwa mnaniamrisha niwafukuze vipenzi vya Allah Mtukufu na nijiepushe nao».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net