Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 28

Hud 11:28

هود

قَالَ يَـٰقَوْمِ أَرَءَيْتُمْ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّى وَءَاتَىٰنِى رَحْمَةً مِّنْ عِندِهِۦ فَعُمِّيَتْ عَلَيْكُمْ أَنُلْزِمُكُمُوهَا وَأَنتُمْ لَهَا كَـٰرِهُونَ

Maana

Akasema, "Enyi kaumu yangu! Hebu fikirini! Ikiwa mimi ninayo hoja wazi iliyotoka kwa Mola wangu Mlezi, na amenipa rehema kutoka kwake, nayo ikafichwa kwenu. Je, tuwalazimishe kuikubali ilhali nyinyi mnaichukia?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Akasema: Enyi watu wangu! Hebu fikirini! Ikiwa mimi ninayo hoja wazi iliyo toka kwa Mola wangu Mlezi, na amenipa rehema kutoka kwake, nayo ikakufichikieni; je, tukulazimisheni kuikubali hali nyinyi mnaichukia? [28]

[28] Nuhu akasema: Enyi watu! Hebu nambieni, ikiwa mimi naungwa mkono na hoja zilizo wazi kutokana na Mola wangu Mlezi, naye akanipa kwa rehema yake Unabii na Utume, na nuru yake ikafichikana kwenu, na kughurika kwenu kwa cheo na mali kukakutieni upofu msizione, basi je, itafaa tukulazimisheni mziamini hoja kwa nguvu na karaha?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Nûḥ akasema, Enyi watu wangu, iwapo mimi niko kwenye hoja iliyo wazi kutoka kwa Mola wangu katika yale niliyokuja nayo kutoka Kwake, itawafunukia nyinyi kwamba mimi niko kwenye haki inayotoka Kwake na kwamba Ameniletea rehema kutoka Kwake, nayo ni unabii na utume na kwamba Allah Mtukufu Amewafichia hayo kwa sababu ya ujinga wenu na kuhadaika kwenu. Basi je kwani inafaa niwalazimishe nayo kwa nguvu hali nyinyi mnaikanusha? Hatutafanya hivyo, lakini tunayategemeza mambo yenu kwa Allah Mtukufu ili Atoe uamuzi Anaoutaka kuhusu mambo yenu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net