Hud 11:27
هودفَقَالَ ٱلْمَلَأُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِن قَوْمِهِۦ مَا نَرَىٰكَ إِلَّا بَشَرًا مِّثْلَنَا وَمَا نَرَىٰكَ ٱتَّبَعَكَ إِلَّا ٱلَّذِينَ هُمْ أَرَاذِلُنَا بَادِىَ ٱلرَّأْىِ وَمَا نَرَىٰ لَكُمْ عَلَيْنَا مِن فَضْلٍۭ بَلْ نَظُنُّكُمْ كَـٰذِبِينَ
Basi wakasema wakuu waliokufuru katika kaumu yake, "Hatukuoni wewe isipokuwa ni mtu tu mfano wetu, wala hatukuoni wamekufuata isipokuwa wale wetu walio duni, watu wasiokuwa na maoni. Wala hatuwaoni nyinyi kuwa mna ubora wowote kutushinda sisi. Bali tunawadhania nyinyi kuwa ni waongo."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wakasema wakuu walio kufuru katika kaumu yake: Hatukuoni wewe ila ni mtu tu kama sisi, wala hatukuoni wamekufuata ila wale walio kuwa kwetu watu duni, wasio kuwa na akili. Wala hatukuoneni kuwa mna ubora wowote kutushinda sisi. Bali tuna hakika nyinyi ni waongo. [27]
[27] Wakuu wa kaumu yake wakasema: Sisi hatukuoni wewe ila kuwa ni mtu kama sisi. Hapana lolote linalo kufanya uwe namna ya peke yako, au uwe na ubora wa kutupelekea tukuamini kuwa wewe ni Mtume utokaye kwa Mwenyezi Mungu! Na wala hatuwaoni hao walio kufuata ila ni watu wa t'abaka la chini miongoni mwetu! Wala hatukuoneni nyinyi kuwa ni bora kuliko sisi! Bali sisi tunaitakidi kuwa nyinyi ni waongo tu katika hayo mnayo dai.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wakasema wakubwa wa ukafiri miongoni mwa watu wake, Wewe si Malaika bali wewe ni binadamu, inakuwaje wewe uletewe wahyi bila sisi? Na hatukuoni umefuatwa isipokuwa na wanyonge wetu, na wao wamekufuata bila kufikiria wala kupima. Na sisi hatuwaoni nyinyi kuwa muna ubora wowote juu yetu, wa riziki wala mali, tangu mlipoingia kwenye dini yenu hii. Bali sisi tunaamini kwamba nyinyi ni warongo katika madai yenu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net